Tuesday, January 29, 2013

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI, KAMISHNA JENERALI JOHN MINJA AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA UDEREVA .

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (katikati) akikagua gwaride la heshima la wahitimu wa mafunzo ya awali ya udereva wa magari kozi namba 18 na udereva wa matreka kozi namba 7 katika Chuo cha Udereva na Ufundi cha jeshi hilo (KPF) kilichopo Kingolwira nje kidogo ya Mji wa  Morogoro.  
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake na baadaye kufunga mafunzo hayo ya awali.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimpongeza Beatrice Dugange baada ya kumpa cheti na leseni ya udereva baada ya kumaliza mafunzo ya udereva chuoni hapo. Jumla ya wanafunzi 66 walipatiwa vyeti na leseni kwa kuhitimu mafunzo hayo.  
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkono wa Mara iliyopo chuoni hapo wakitumbuiza katika sherehe hiyo kwa kutoa michezo mbalimbali mbele ya mgeni rasmi, Kamishna Jenerali John Minja.
Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza kwa makini, Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja wakati akitoa hotuba yake na baadaye kuyafunga mafunzo ya  udereva wa magari kozi namba 18 na udereva wa matreka kozi namba 7.PICHA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI.

No comments: