Saturday, January 26, 2013

UPDATE, KUTOKA MTWARA, Nyumba ya Mkuchika inawaka moto-Newala, Gereza lavamiwa wafungulia wafungwa.


 Taarifa za redio mbao ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa  ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na kisha kupiga moto gereza. Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.

Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu. Maaskari na makachero wamewasili  Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.

1 comment:

Anonymous said...

Hao wananchi wa mtwara watumie busara na akili kuchoma nyumba moto na kuanzisha vurugu haitasaidia chochote zaidi ya kusababisha hasara na kupoteza maisha ya watu!