Wednesday, February 20, 2013

ALBINUS KUGOMBEA UBINGWA WA DUNIA WA IBF KWA VIJANA

Bondia kijana na anayeinukia kwa kasi Albinu Felesianu (kulia) wa nchi ya Namibia amepewa ofa ya kugombea ubingwa wa dunia wa Featherweight kwa vijana walio chini ya miaka 25 unaotambuliwa na IBF. Albinus amezoea kupewa zawadi za Christmas na siku kuu yake ya kuzaliwa lakini hamna kilichomwandaa na mshtuko mkubwa ambao aliupata wakati IBF ilipotangaza hivi karibuni kuwa imempatia nafasi ya kugombea mkanda wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25. Mtua ambaye anaweza kuiua furaha yake ni mmoja wa watoto wa Nkrumah, Mghana Ishmael Ayeetey ambaye amekulia katika moja ya viunga vinavyosifika kwa kutoa mabingwa wa ngumi wa dunia kama kina Azumah Nelson, Joseph Agbeko na Ike Quartey.

No comments: