Tuesday, February 5, 2013

BALOZI SEIF AZINDUA MIRADI MBALIMBALI SINGIDA.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na salama Mkoani Singida Mhandisi Issac Nyankonji  akitoa maelezo ya hatua za ujenzi wa mradi wa maji safi mkoani humo mbele ya Balozi Seif ambaye alikuwa akiangalia utekelezaji wa ilanini ya CCM akiwa mlezi wa Chama hicho wa Mkoa huo.
Mlezi wa CCM Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mkinya Mwalimu Jonson Kilinga, mchango wa shilingi 500,000/- , vyakula pamoja na Mabegi kwa ajili ya wanafunzi wa Shule hiyo.
Mlezi wa CCM Mkoa wa SingidaBalozi Seif Ali Iddi, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Jengo la Maabara ya Shule ya Sekondari ya Mkinya  Wilaya ya Dung’unyi Mkoani Singida.
Mlezi wa CCM Mkoa wa Singida Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, akiweka jiwe la msingi la Saccos ya Kijiji cha Mkinya Mkoani Singida alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoani humo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akiwa pamoja na Viongozi wa CCM wa Mkoa wa Singida wakiwa katika harakati za kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji safi Mkoani humo ikiwa utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2010/2015.

No comments: