Sunday, February 10, 2013

CHAMA CHA AKIBA NA KUKOPA CHA JESHI LA MAGEREZA NCHINI (TPS-SACCOS) CHAPATA VIONGOZI WAPYA, MJINI MOROGORO.

Baadhi ya viongozi wapya waliochaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Akiba na Kukopa cha Jeshi la Magereza (TPS Saccos) wakiwa mbele ya wajumbe hao (hawapo pichani). Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Joel Bukuku akizungumza na wajumbe hao. Uchaguzi huo umefanyika katika Hoteli ya Edema, mjini Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifurahia kupata viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho.
Wajumbe wa Bodi ya TPS Saccos waliomaliza muda wao wakiondoka meza kuu na kuupisha uongozi mpya. Kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dionece Chamulesile, wa katikati ni Dk Juma Malewa na Stanford Ntirundura waliokuwa wajumbe wa bodi hiyo
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Dionece Chamulesile akitoa hotuba ya kuufunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pili wa TPS Saccos uliofanyika mjini Morogoro.

No comments: