Wednesday, February 13, 2013

CHEKA KUZICHAPA NA THOMAS MASHALI.

 Francis Cheka (kushoto) akiwa na Adam Tanaka (katikatia) na Thomas Mashali (kulia)         SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa) limetoa kibali kwa bondia Francis Cheka ambaye ni bingwa wa Africa katika uzito wa Super Middle kutetea ubingwa wake dhidi ya bondia Thomas Mashali wa Tanzania. Mabondia hao wawili leo tarehe 13 February walikutana katika hoteli ya Ndekha, iliyoko Magomeni Kondoa na kutia saini mkataba wa kupigana pambano hilo ambalo limepangwa kufanyika siku ya Mei Day katika ukumbi wa PTA jijini dar-Es-Salaam. Thomas Mashali ambaye ndiye bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle anakiwango kizuri cha kushindana na Francis Cheka katika pambalo hilo. Hii itakuwa mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea mkanda alioushinda tarehe 29 April 2012 dhidi ya bondia machachari Mada Maugo wa Tanzania. Cheka aliutetea vyema mkanda wa ubingwa wa IBF/Africa dhidi ya bondia Chiotcha Chimwemwe ambaye ni Afisa katika jeshi la Malawi siku ya Boxing Day (26 Decewmber 2012) katika jiji la Arusha. Kama Francis Cheka atashinda tena pambano hili, atapewa nafasi ya kupigana kugombea mkanda wa IBF wa mabara (IBF I/C).Pambano hili linaandaliwa na kampuni ya Mumask Investment and Gebby Pressure ya jijini Dar-Es-Salaam chini ya uratibu wa Adam Tanaka!Imetumwa na: UONGOZI, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa), Dar-Es-Salaam, Tanzania

No comments: