Wednesday, February 20, 2013

DK.SHEIN AMUAGA PADRI EVARIST GABRIEL MUSHI KWA SAFARI YAKE YA MILELE..

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein, (kushoto) akitoa salamu ya Mwisho kwa mwili wa Marehemu Padri Evarest Mushi, katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar, Padri Gabriel Mushi, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita,na atazikwa leo Kijini Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja, (katikati) Askofu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Zanzibar Augustino Shao
Dk.Shein akisalimiana na viongozi wa kanisa hilo alipofika kuaga mwili wa marehemu huyo
Akisalimiana na watu mbalimbali waliofika kwenye maombolezo na kuaga mwili wa marehemu huyo.

Dkt.Ali Mohamed Shein,akitia saini kitabu cha maombolezi ya Padri Evarist Gabriel Mushi,katika Kanisa la Minaramiwili Mjini Zanzibar,ambapo alifika kutoa salamu ya mwisho kwa Padri huyo, aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikana Jumapili iliyopita.
Waombolezaji mbalimbali waliofika kuaga mwili wa marehemu huyo.

No comments: