Wednesday, February 6, 2013

DK.SHEIN APOKEA MIPIRA KWAAJILI YA KUIMARISHA SOKA ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea mpira ukiwa ni miongoni mwa mipira kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Bi.Sharifa Khamis Salim, alipofika Ikulu kukabidhi mipira hiyo pamoja na kamati ya ugawaji mipira hiyo,kutoka mradi wa "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRIKA", hafla hiyo  ilifanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Kamati ya ugawaji Mipira kutoka mradi wa "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRIKA", chini ya Mwenyekiti wake Bi.Sharifa Khamis Salim, pia akiwa  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo, hafla hiyo ilifanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Katibu wa Kamati ya Ugawaji wa Mipira ya Mradi wa "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRIKA", Khamis Abdalla Said,akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati kamati hiyo ilipofika Ikulu Mjni Zanzibar kukabidhi Mipira kwa Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo.

No comments: