Tuesday, February 26, 2013

GOOGLE NA COMPUTER YA MIWANI: KUANZA KUUZWA 2013.

Google ni ulimwengu wa uvumbuzi wa bidhaa na majaribio ya teknolojia, katika baadhi ya mawazo na uvumbuzi ambao Google wanaendelea kufanyia kazi kuna mambo ambayo sio ya kufirika, gari inayojiendesha na kompyuta ya kuvaa kama miwani ni miongoni mwa teknolojia hizo, kwa mtazamo wa haraka unaweza kudhani kuwa itachukua miaka zaidi ya 10 Google kuweza kuziuza bidhaa hizo kwa watu wa kawaida.

Ukweli ni kwamba Google imeshatangaza kuwa Google Glass itaanza kuuzwa mwaka huu wa 2013. Google Glass ni kompyuta ambayo huvaliwa kama miwani na ina uwezo na matumizi mbali mbali kama vile kurekodi video na kupiga picha. Katika ongezo jipya la Google Glass ni kwamba kompyuta hiyo itaweza kutumia amri za sauti (voice command), kuanzisha amri ya sauti unatakiwa kuiambia miwani hiyo “OK Glass” na miwani itaanza kukusikiliza unataka ifanye nini kabla ya kuipa amri kama vile “record video”. Pia Google wameonyesha baadhi ya matumizi ya miwani hiyo ambayo ni ya kawaida kabisa mbali na yale ya kuchupa na parashuti kutoka kwenye ndege.

No comments: