Friday, February 8, 2013

HUDUMA ZA DUTY FREE SHOPS KATIKA JESHI LA MAGEREZA YAZINDULIWA.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shop, Afzal Meghji akimuonyesha bidhaa mbalimbali zilizopo ndani ya duka la kwanza kwenye Supermarket ya Magereza, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, mara baada ya kufungua Supermarket hiyo kubwa na yakisasa itakayowawezesha askari magereza na familia zao kupata bidhaa kwa bei nafuu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmauel Nchimbi akipokea zawadi kutoka kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan Virji (kulia).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na maafisa magereza (hawapo pichani) kabla ya kufungua Supermarket kubwa ya kisasa ambayo itawawezesha maafisa hao, askari na familia zao kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na kulia ni Mwekezaji Mkuu wa Kampuni ya Military Shops ambaye ndiye aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Sadrunin Virji. 
Baadhi ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa mbalimbali katika Supermakert hiyo baada ya kuzinduliwa.

No comments: