Saturday, February 16, 2013

JAJI MKUU WA KENYA AKUTANA NA TUME YA KATIBA MPYA NCHINI.

Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) akibadishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume, Dkt. Sengondo Mvungi nje ya ukumbi wa Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume. Mhe. Mutunga alikutana na Wajumbe ili kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba Mpya.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,  Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (kushoto) akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga nje ya ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume jana, Mhe. Mutunga amekutana na Wajumbe wa Tume kubadilishana mawazo na uzoefu wake kuhusu uandishi wa  Katiba Mpya.

No comments: