Wednesday, February 20, 2013

KAPUMZIKE KWA AMANI!

Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Ali Mohamed Shein, (katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki  wakiwa katika mazishi ya marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja, ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa.
Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi akitia udongo  katika kaburi la Marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo  katika viwanja vya kanisa la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi,akiongoza  sala  wakati wa mazishi ya  Marehemu  Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya kaskazini B Unguja leo.
Askofu wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel  Mushi,aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo, kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu  Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo  katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja, ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa.

No comments: