Saturday, February 23, 2013

KUSITISHWA KWA MAANDAMANO YA CUF NA SABABU ZA KUFANYA MAANDAMANO HAYO!

Polisi wakiwa katika Doria kuhakikisha Maandamano hayafanyiki mjini Lindi jana.
Safari ya doria ilianzia hapa kwenye eneo la Kituo Cha Polisi.
Kwenye kituo cha mabasi.
Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Lindi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini,Salum Barwany akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani)
.Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,George Mwakajinga akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani)
KUSITISHSHWA kwa maandamano hayo kunafuatia barua ya Kamanda wea Polisi wilaya ya Lindi ya tarehe 20 mwezi huu kwa Chama hicho cha CUF Kuyakataa maombi yao ya kutaka kufanya maandamano makubwa na mkutano wa Hadhara

Katika barua hiyo Cuf ilitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Lindi ya kutaka kufanyika maandamano makubwa na mkutano wa Hadhara kwa lengo la kuishinikiza serikali kutoa tathmini ya Maendeleo ya Miradi
ya Gesi asilia,Maji,Stakabadhi ghalani pamoja kupatiwa taarifa ya kuanza kutekelezwa kwa ahadi za serikali juu ya ujenzi wa viwanda vitavyotokana na gesi na kuitafsiri mikataba ya gesi

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na suala hilo la Maandamano Mbunge wa chama hicho ambae pia ni Mwenyekiti wa Wilaya,Salum Barwany amesema chama chake kimelazimika kusitisha maandamano hayo kwa muda hadi tarehe 03 mwezi ujao na kusisitiza kwamba maandamano ni haki ya Msingi kuwawezesha wananchi kutoa kero zao
 

Sambamba na hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga ameeleza kuwa Ofisi yake imeamua kuzuia maandamano hayo kufuatia Mialiko mbalimbali iliyotolewa kwa mkoa wa Mtwara ambako hivi karibuni kulitokea hali ya uvunjifu wa Amani na kusababisha Vifo,uchomaji wa moto kwa nyumba za wabunge na serikali ikiwemo magari
‘’Maandamano ni haki ya msingi kwa vyama vya siasa ila inatushangaza unapotoa mialiko kwa mikoa mingine hii imetuweka njia panda inakuwaje maandamano ya Lindi waje na Mtwara hii Hapana ni lazima Jeshi lijipange ndio tutaruhusu kwa kuwa tetesi tulizozipata wengine wanakuja kwa ajili ya Fujo..alimalizia Kamanda Mwakajinga

No comments: