Thursday, February 21, 2013

MTANDAO WA KUDHIBITI MALARIA (TANAM) WAJENGA NGOME MKOANI LINDI.

Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Uchumi Mkoa wa Lindi,Bw John Likangoakikabidhi pikipiki kwa viongozi wa asasi za kiraia Mkoani Lindi kwenye Hafla Fupi iliyofanyika mkoani humo jana.
Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Uchumi Mkoa wa Lindi,Bw John Likango (katikati) akijaribu kuwasha moja ya pikipiki hizo.
 Abdulaziz,Lindi
MTANDAO wa kudhibiti Malaria Nchini(TANAM) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Chini ya Ufadhili wa Global Fund imekabidhi Jumla ya pikipiki 14 kwa Asasi mbalimbali za kanda ya Kusini ikiwa ni jitihada za
kuelimisha Jamii jinsi ya kupigana na adui malaria  ambapo tayari Asasi hiyo ikiwa imefikisha elimu mpaka ngazi ya Kata ikiwa pamoja na Utunzaji wa Mazingira. 

Pamoja na lengo la serikalila  kujenga zahanati katika kila kijiji na kituo cha afya kwenye kila kata nchi nzima imelezwa kuwa elimu ikitolewa ya udhibiti wa Ugonjwa huo kwa  wananchi itasaidia zaidi kupunguza ugonjwa huo, kabla ya kujenga zahanati na vituo vya afya ikiwemo Ugawaji wa Vyandarua.
Akizungumza mara Baada ya kukabidhi Pikipiki kwa Asasi za Mkoa wa Lindi na Mtwara pamoja na Ya Mratibu wa Mtandao wa kudhibiti Malaria kanda ya Kusini Katika hafla fupi iliyofanyika Leo, Katibu Tawala Msaidizi Huduma za Uchumi Mkoa wa Lindi,Bw John Likango sambamba na kutoa wito kwa Asasi hizo juu ya Matumizi ya Pikipiki hizo alieleza kuwa Udhibiti wa Malaria utafanikiwa ikiwa Elimu itatolewa zaidi kupunguza vyanzo vya Ugonjwa huo hapa Nchini Aidha mwakilishi wa Mtandao Huo toka Makao Makuu,Bw Sunny Kuluvia sambamba na kutoa Pikipiki hizo aliwaomba wananchi kutoa Ushirikiano
ambapo wakielimishwa kuhusu malaria, watafahamu njia sahihi ya kupambana nayo, ikiwemo kusafisha mazingira ili kuua mazalia ya mbu wanaoambukiza ugonjwa huo hatari kwa jukumu ni lao kushirikiana na
Serikali
  Kwa upande wake Katibu wa Asasi ya Lisawe ya Mjini Lindi Bi Prisisca Unga alieleza jinsi watakavyo shirikiana na Jamii kupitia mawakala wa Kata kurahisisha utoaji wa elimu baada ya kupewa Usafiri
Kupitia Mpango jumla ya pikipiki 55 zimenunuliwa kwa ajili ya kanda Tatu zilizo katika mpango huo Nchini huku tayari pikipiki kwa Asasi 13 za Mkoa wa Lindi na Mtwara zimekabidhiwa ambapo Asasi hizo ni Lisawe Ya Lindi Mjini, Shikwauki-Kilwa, Ropa-Ruangwa, Mukemba-Mtwara vijijini,Masha-Mtwara/Mikindani,FEM-Lindi Vijijini, Naeso-Nachingwea,Lifa-Liwale,Lefe-Nanyumbu,Neda-Newala,Shikum-Masasi na TWA ya Tandahimba zimekabidhiwa ili kusaidia utoaji wa Elimu kwa

Jamii

No comments: