Sunday, February 3, 2013

MWAKA MPYA WA KICHINA KUKARIBISHWA LEO JIJINI DAR.

Makamu Meya wa Manispaa ya   Tianjin kutoka China  Bi. Zhang  Junfang, (kushoto) akikabidhi picha ya kiutamaduni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.Fenella Mukangara wakati alipomtembelea leo ofisi kwake jijini Dares Salaam, ikiwa ni ishara ya ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi yake na Tanzania. Meya huyo yuko nchini kwa ajili ya sherehe za mwaka wa Kichina zitakazo adhimishwa leo jioni kwenye uwanja wa Mnazimmoja, Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin kutoka China  Bi. Zhang  Junfang, (watatu kushoto) akifurahi baada ya kumvalisha kitambaa (skafu) chenye michoro ya utamaduni wa China leo jijini Dar es Salaam. Meya huyo yupo nchini kwaajili ya sherehe ya mwaka mpya wa Kichina itakayofanyika leo jioni kwenye uwanja wa Mnazimmoja, Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Makamu Meya wa Manispaa ya   Tianjin kutoka China  Bi. Zhang  Junfang, (katikati ) akimvisha kitambaa chenye michoro ya  kiutamaduni, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.Fenella Mukangara wakati apomtembelea leo ofisi kwake jijini Dares Salaam, ikiwa ni ishara ya ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi yake na Tanzania.Meya huyo yuko nchini kwa ajili ya sherehe za mwaka wa Kichina zitakazoadhimishwa leo jioni kwenye uwanja wa Mnazimmoja, Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Meya huyo akizungumza na Waziri wa habari. Picha na magreth kinabo - maelezo

No comments: