Thursday, February 7, 2013

WAMA YAPIGA JEKI HOSPITALI YA SOKOINE, Vifaa vya Tsh700Millioni vyakabidhiwa.

Mwenyekiti wa Taassi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ambaye pia ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati) akikata utepe kuzindua baada ya vifaa tiba vilivyo kabidhiwa na taasisi yake kwa kushirikiana na Taasisi ya Project Cure ya Marekani kwa Hospitali ya Mkoa wa Lindi Sokoine mkoani humo leo. Jumla ya vifaa vyenye thamani ya Tsh700Millioni vilikabidhiwa. Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na Mashine ya X-ray pamoja na vifaa vyake vyote, Mitambo ya kitanda maalum cha ICU Kwa ajili ya wagonjwa mahututi, Mitungi ya gesi ya Oxygen ambayo itasaidia kutoa huduma ya dharura hasa wakati Umeme umekatika,Vifaa na mitambo kwa ajili ya huduma za kinywa na meno,Vifaa vya upasuaji mdogo na mkubwa,Ultra sound machine, Taa,meza na mashine ya Usingizi
Baadhi ya vifaa vilivyo kabidhiwa.
Mama Salma akipokea kichanga alipotembelea kuona wagonjwa kwenye wadi mbalimbali za Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo.

No comments: