Saturday, February 2, 2013

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MWAMINI MALEMI ATEMBELEA GEREZA MAALUM LA WAFUNGWA WAKOROFI LINALOENDELEA KUJENGWA MJINI DODOMA.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, SACP Kibana Kamtande akimfafanulia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mwamini Malemi (wapili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo, Agnela Nyoni (kulia) jinsi ujenzi wa gereza hilo ulivyoanza na unavyoendelea.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiwa na maafisa wa jeshi hilo ndani ya gereza hilo ambalo linaendelea kujengwa.
Injinia wa Ujenzi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma, Salum Omari akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (kushoto) maeneo mbalimbali ya gereza maalum la wafungwa wakorofi linaloendelea kujengwa karibu na Gereza la Isanga mkoani Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Jeshi hilo nchini, Kamishna Jenerali John Minja.
Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi akiwauliza maswali mbalimbali maafisa wa magereza na baadaye kuwataka kusimamia vizuri ujenzi wa gereza hilo ambalo litakuwa la kwanza nchini kwa ajili ya kuwahifadhi wafungwa wakorofi.

No comments: