Saturday, February 16, 2013

NSSF YACHANUA MBAWA ZAKE KWA VIONGOZI WAKUU ZANZIBAR.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Kanda ya Dodoma Maryam Ahmed, akimweleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi juu ya faida za kujiunga na mfuko huo kabla ya kumsajili rasmi kuwa mwanachama wa Mfuko mjini Zanzibar jana. Mkoa wa Dodoma ambao ndio uliopewa jukumu la kuhudumia Viongozi wa ngazi ya Juu Bibi Maryma Ahmed alisema  zaidi ya Wabunge 165 wamekubali kujiunga kwa hiari kuwa wanachama wa Mfuko huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijaza Fomu Maalum ya kuomba uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Balozi Seif Ali Iddi akiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliofika Ofisini kwake Vuga kumsajili rasmi kuwa mwanachama wa mfuko huo.

No comments: