Saturday, February 16, 2013

SHEIKH PONDA ANAVYOLIHENYESHA JESHI LA POLISI NCHINI. Muda wakazi unapotea, Gharama za kuimarisha ulinzi ni kubwa, Swali kuu linabaki palepale Ponda ni nani?

Polisi walivyo imarisha ulinzi nje ya jengo la Sukari lililopo  mkabala na Makutano ya Barabara za Ohio na Sokoine Driver Posta jijini Dar es salaam jengo hilo ndmo zilimo ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikal Dk.Eliezer Feleshi, Ulinzi huo umeimarishwa kutokana na tishio la wafuasi wa Shekh Ponda kutishia kuandamana kwenda kwa Mwendesha Mashtaka huyokushinikiza Shekh Ponda aachiwe huru.


Baadhi ya wafuasi hao wa Shekh Ponda wamekamatwa katika maeneo mbalimbali wakati wakijaribu kuingia katika eneo la Posta ambapo ulinzi mkali uliimarishwa huku polisi wakitumia Magari, Pikipiki, Mbwahuku makachero wakizunguka kila mahali.
Baadhi ya Barabara zilifungwa ili kuweka eneo hilo katika hali ya usalama zaidi na kuhakikisha linzdhibitiwa na kulidwa kirahisi.
Magari ya akiba yalitolewa kuongeza ulinzi.
Walizinguka karibu mitaa yote ya Posta.
Hivi ndivyo ilivyokuwa.
Wafuasi hao wa Shekh Ponda wakipanda kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa katika maandamano hayo.
Zoezi la kuwakamata na kuwapeleka polisi watuhumiwa hao likiendelea chini ya ulinzi mkali.

No comments: