Sunday, February 3, 2013

SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM ZAFANA KIGOMA.


 Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa hotuba yake kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliohudhulia Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma jioni hii.

Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harisson Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii na kuwahakikishia kuwa sasa hivi mkoa wa Kigoma mambo yako vyema kabisa na treni itaendelea kufanyaka kazi kama zamani.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisema machache, muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akiongoza shughuli hiyo.

Chipkizi wa CCM Mkoa wa Kigoma wakifanya Gwaride la heshima kwa Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

No comments: