Tuesday, February 19, 2013

VIONGOZI WA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA (ICTR) WAMTEMBELEA WAZIRI NCHIMBI OFISINI KWAKE.

Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Roland Amoussouga akimfafanulia masuala mbalimbali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) wakati viongozi hao walipomtembelea waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kutoka kushoto ni Msajili wa Mahakama hiyo, Bongani Majola. Kulia ni Mwanasheria wa mahakama hiyo, Jerry Mburi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza ofisini kwake na  Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani Majola (katikati). Ziara hiyo, ambayo pia ilikuwa na lengo la msajili huyo kujitambulisha na kumsalimia Waziri Nchimbi, na kumuelezea shughuli mbalimbali zifanywazo na mahakama hiyo pamoja na kumuelezea changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama hiyo.  Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliahidi kushirikiana na mahakama wakati wowote itakapohitaji msaada kutoka ofisini kwake.
Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani Majola (katikati) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) kuhusiana na mafanikio na changamoto mbalimbali ya Mahakama hiyo ambayo Makao Makuu yake yapo jijini Arusha. Kulia ni Msemaji wa Mahakama hiyo, Roland Amoussouga.

No comments: