Tuesday, February 5, 2013

WAKUU WA MAGEREZA WAPEWA MAFUNZO YA JINSIA.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akipokelewa na Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia kwa wakuu wa magereza wa mikoa yote Tanzania Bara, maafisa waandamizi wa makao makuu, watumishi raia na askari kutoka magereza mbalimbali nchini. Mfunzo hayo ya siku nne yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro.  

Maafisa Magereza wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya jinsia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Mabadiliko ya Sekta ya Sheria nchini, Bi. Wanyenda Kutta baada ya kumkabidhi taarifa ya hali ya Utekelezaji wa Masuala ya Jinsia katika  Taasisi zinazotekeleza Programu ya Maboresho ya Sekta hiyo.

No comments: