Friday, February 8, 2013

ZANZIBAR WALIVYOADHIMISHA SIKU YA SHERIA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, (kushoto) na Kaimu Waziri wa Katiba na Sheria pia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui, alipowasili katika viwanja vya Victoria Garden, katika Maadhimisho ya  Siku ya Sheria Zanzibar, zilizofanyika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (wa tatu kushoto) Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Fakih Jundu, (kutoka kushoto) na Kaimu Waziri wa Katiba na Sheria, pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui, (kutoka kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi khamis, Spika wa baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, wakiangalia Kikundi cha wasanii cha Black Roots kilipokua kikitumbuiza katika kilele cha Siku ya Sheria.
Baadhi ya Makadhi wa walioalikwa  katika Maadhimisho ya  Siku ya Sheria,katika uwanja wa Bustani ya Victoria Garden, wakifuatilia kwa makini harakati za maadhimisho hayo zilivyoendelea na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akionesha jarida la Mahakama baada ya kulizindua wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar, zilizofanyika leo, katika viwanja vya Victoria garden Mjini Zanzibar, (kushoto), Kaimu  Waziri wa Katiba na Sheria, pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui na  Jaji Mkuu wa
Zanzibar Omar Othman Makungu
(kulia)

No comments: