Wednesday, March 13, 2013

BALOZI WA UMOJA WA ULAYA (EU) NCHINI AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, DK EMMANUEL NCHIMBI OFISINI KWAKE, JIJINI DAR ES SALAAM.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi (katikati). Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. Balozi huyo alipofanya ziara ya kikazi wizarani hapo, jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi (katikati) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima wakati balozi huyo alipofanya ziara ya kikazi wizarani hapo, jijini Dar es Salaam kuhusiana na ushirikiano kati ya EU na wizara hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi (katikati) kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya EU na wizara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
No comments: