Saturday, March 16, 2013

DC RUANGWA ATAKA FEDHA ZA BIMA YA AFYA ZITUMIKE KUNUNULIA DAWA.

Wadau mbalimbali wakishiriki semina Kuhusiana na mfuko wa afya ya jamii CHF Wilayani RUANGWA
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Lindi, BI fortunata Raymond (kushoto) akikabidhi msaada wa mashuka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Agness Hokororo, kwaajili ya Hospital ya wilaya hiyo, Kulia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa, Mfune akishuhudia tukio hilo

Mkuu wa wilaya pamoja na Meneja wa Nhif Lindi wakitandika moja ya shuka zilizokabidhiwa
Abdulaziz video,Ruangwa
MKUU wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi Agnes Hokororo amemtaka mganga mkuu wa wilaya hiyo kuzitumia fedha za mfuko  wa afya ya jamii kununulia dawa na  vifaa  tiba  ili kuondoa upungufu wa madawa
unazozikabili zahanati na vituo vya afya mara kwa mara katika wilaya hiyo.
Wito huo ameutoa wakati alipokuwa anafungua  mafunzo ya  elimu ya kata kwa kata kwa wadau na wanachama wa mfumo wa taifa bima ya afya na jamii uliofanyika  wilaya ruangwa jana. hokororo alisema kuwa kero nyingi zinatolewa na jamii kuhusiana na huduma za mbovu zinazotolewa kwenye baadhi ya vituo  vya  afya, zahanati, inasababishwa na watendaji wasio waadilifu katika sekta ya afya kwa ukosefu wa dawa wilayani humo.
Alisema wapo watumishi  wachache  wenye  malengo  ya kuvipaka  matope vituo vya kutolea huduma kwa sababu zao binafsi na imani potofu kuwa wanachama wa mfuko wa  bima ya afya  ni wagonjwa wanaopata huduma bure.
Aidha alifafanua kua ni wajibu wa watoa huduma  wa sekta ya afya kuwa wabunifu na kuzingatia wajibu wao, maadili  na kufuata  masharti yaliyowekwa na serikali ili waendelee kujijengea heshima  na kulinda  heshima za sekta ya afya.

No comments: