Sunday, March 10, 2013

DK.SHEIN ALIPOFUNGA ZIARA YAKE WILAYA YA KATI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimtwisha ndoo ya maji Asha Mohamed Abdulla, wa Kijiji cha Chwaka,mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji Safi na Salama, Sherehe ya ufunguzi wa Mradi huo umefanyika Kijijini hapo jana, alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua bomba la maji  kuzinduia Mradi wa Maji Safi na Salama wa Kijiji cha Chwaka,Wilaya ya Kati Unguja, alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini jana.
Wazee wa Kijiji cha Chwaka wakiwa na fuaraha kubwa na kumsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa sherehe
ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi na salama Kijijini hapo jana alipokuwa katika ziara ya kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chwaka,Wilaya ya Kati Unguja,wakati wa sherehe ya uzinduzi
wa Mradi wa Maji Safi na salama jana.

No comments: