Saturday, March 9, 2013

DK.SHEIN ALIPOHUDHURIA MAULID TEMEKE JIJINI DAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wapili kushoto) akiwaongoza Viongozi mbali mbali kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, (watatu kushoto) ni Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akifuatiwa na Reginald Mengi na Shamsi Vuai Nahodha katika Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid  Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Sheikh Alhad Mussa Salim, alipowasili katika msikiti Masjid Majmuatil Islamia, wa Temeke mwisho kuhudhuria katika maulid ya Mtume Muhamad (SAW).
Sheikh,Dk.Usama Mohammed Esmail, kutoka nchini Misri akitoa mawaidha wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad SAW, yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid  Majmuatil Islamia, wa Temeke mwisho, yaliyohudhuriwa na Viongozi wa Dini mbali mbali,na mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Wanafunzi wa Madrasatul Az-har ya Koma Kisiwani Mafia, wakisoma Qaswida Ya swalatu Alan Nabii, jijini Dar es Salaam, katika Maulid ya Kumswalia Mtume Muhammad (SAW), yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid  Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Jijini Dar es Salaam, waliohudhuria katika Maulid ya Kumswalia Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika jana yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid  Majmuatil Islamia wa Temeke mwisho.
Ustadh Abbas Hamdani wa Kinondoni,akisoma utenzi wakati waMaulid ya  Kumswalia Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika jana katika Msikiti Masjid  Majmuatil Islamia,wa Temeke mwisho. .[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments: