Friday, March 8, 2013

HALI YA HEWA JIJINI DAR LEO, Mvua yatuma salamu mabondeni. Yanyesha kwa mgao kama umeme.

Mwonekano wa baadhi ya mitaa leo jijini Dar es Salaam kutokana na kutanda kwa wingu la mvua huku baadhi ya maeneo ikinyesha na kusababisha usumbufu kwa baadhi ya wakazi wa jiji hilo. Pichani ni eneo la barabara ya Kawawa eneo la karibu na Moroco Hotel.
Kufuatia mvua zilizoanza kunyesha eneo la Jangwani limeanza kufurika maji hali inayoashiria hatari kwa wakazi wa karibu na eneo hilo kutokana na hatari ya mafuriko. Mwakajana eneo hilo la Jangwani kata ya Suna lilikumbwa na mafuriko hali iliyosababisha familia zaidi ya 500 kukosa mahala pakukaa.
Moja ya mito inayotiririsha maji kutoka maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuelekea Jangwani ukiwa umefurika maji ambayo hayatembei kutokana na mito hiyo kuziba hali inayoweza kuharakisha mafuriko kusambaa hadi maeneo ambayo hayatarajiwi kufikiwa na mafuriko.
Pamoja na hatari na hofu iliyopo ya mafuriko vijana hawa bila kujali hilo wako kando ya mto  huo haikueleweka walikuwa wakitafuta nini huku wakiwa wamesima juu ya takataka zilizo ondolewa kwenye mto huo kwenye bonde lainalounganisha Kinondoni Mkwajuni na Magomeni.No comments: