Thursday, March 7, 2013

KITUO CHA FEDHA CHA BENKI KUU CHAFUNGULIWA PEMBA.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi kituo cha kutunzia na kusambazia fedha cha Benki Kuu ya Tanzania katika jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar Chake chake Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,  sambamba na Viongozi wa Taasisi za Fedha akiwapungia mkono Wananchi wa Chake chake (hawako pichani) mara baada ya kufungua kituo cha kutunzia na kusambazia fedha cha BOT katika jengo la Benki ya Watu wa Zanzibar  (PBZ) Chake chake Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Watu wa Zanzibar  (PBZ) Nd. Juma Amour Mohammed, alipowasili kwenye ofisi za PBZ Chake chake Pemba kufungua kituo cha kutunzia na kusambazia fedha cha BOT.

No comments: