Friday, March 1, 2013

MAGEREZA KUTENGENEZA KOFIA NGUMU (HELMET) NCHINI.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna John Minja akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum (aliyevaa nguo nyeusi) maeneo mbalimbali yaliyopo nje ya kiwanda hicho.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum moja ya kofia ngumu zitakazokuwa zinatengenezwa kiwandani hapo.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akimsalimia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum kabla ya Mkurugenzi huyo kuingia ndani ya  Kiwanda cha Magereza kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam kukagua maandalizi mbalimbali ya uanzishwaji wa kiwanda hicho. Kulia ni Mdhibiti wa Shirika la Magereza, John Masunga.

No comments: