Friday, March 8, 2013

NSSF yamwaga vifaa vya Michezo kwa timu za vyombo vya habari leo.

Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki michuano ya NSSF Media Cup 2013.
Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto) akimkabidhi nahodha wa Free Media FC, Salum Mkandemba sehemu ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya NSSF Media Cup 2013 yanayoanza kutimua vumbi Jumamosi Machi 9 kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa timu ya TBC, Chacha Maginga akipokea jezi pamoja na viatu kutoka kwa Meneja Uhusiano, Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume. Katikati ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF Juma Kintu.

No comments: