Saturday, March 16, 2013

UJUMBE WA JUMUIYA YA AL RAHMA WAKUTANA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR.

Mwakilishi wa Kampuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi ya Nchini Ras Al- Khaimah Bwana Kamal Ahaya akiuongoza ujumbe wa Jumuiya ya Al-Rahma ya Umoja wa Falme za Kiarabu { UAE } wakati ulipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na Ujumbe wa Jumuiya ya Al-Rahma ukiongozwa na Mwakilishi wa Kampuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi ya Nchini Ras Al-Khaimah Bwana Kamal Ahaya.
Ujumbe huo upo Zanzibar kukagua Vijiji vyenye mazingira magumu ili kuvipatia msaada wa kuviwezesha kuwa na huduma muhimu na za msingi katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

No comments: