Wednesday, March 6, 2013

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, DK EMMANUEL NCHIMBI AKUTANA NA MAWAZIRI NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA NA UTAMADUNI.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati meza kuu) akizungumza jambo alipokutana na Mawaziri wenzake kutoka Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (kushoto kwa Dkt Nchimbi) na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kulia). Mawaziri hao pamoja na Watendaji wakuu kutoka Wizara zao walikutana katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani kujadili kwa pamoja changamoto zinazozikabili Wizara zao katika kuimarisha amani na mshikamano wa nchi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Generali, Said Mwema akizungumza jambo kwenye Mkutano uliowakutanisha Viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya  Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.  Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano, Prof.  John Nkoma.

No comments: