Tuesday, May 28, 2013

SERIKALI YA ZANZIBAR KUFADHILI MAFUNZO YA UDAKTARI.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwalimu Mkuu wa chuo cha Afya Kisiwani Pemba Dr. Maria Magdalena, alipotembelea Chuoni hapo ambapo alitoa kauli ya serikali kwamba itakuwa tayari kumgharamia mwanafunzi yeyote atakayeamua kujiongezea  taaluma ya fani yoyote ya Udaktari Bingwa kwa lengo la kuiondoshea Zanzibar uhaba wa Madaktari.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wanafunzi  12 wa Chuo cha Afya wanaosomea fani ya Udaktari waliopo Kisiwani Pemba.
Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Afya Pemba Dr. Maria Magdalena akielezea furaha yake kutokana na umahiri wa wanafunzi wake mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipowatembelea kwenye makazi yao Wawi Pemba.
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo cha afya Kisiwani Pemba Ali Omar Khalifa, akitoa baadhi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi wa chuo cha afya waliopo Kisiwani Pemba.

No comments: