Saturday, August 10, 2013

BAADA YA KUPIGWA RISASI: PONDA ANATIBIWA MAFICHONI NA MADAKTARI WA KIISILAMU.

JESHI la Polisi Mkoani Morogoro limemtandika risasi ya bega Sheikh Ponda Issa Ponda jana majira ya saa 12:00 jioni baada ya kukataa kutekeleza amri ya kuondoka na askari hao ndipo walipolazimika kutumia nguvu na kufyatua risasi.

 “Tukio limetokea kweli na kulikuwa na matumizi ya nguvu ikiwemo mabomu ya machozi na ufyatuaji wa risasi kutoka kwa askari polisi lakini mhadhara wake haukuwa na fujo yoyote,” walisema watoa taarifa hao.
 Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa zilisema kuwa polisi walifyatua risasi zilizompata kiongozi huyo begani lakini wafuasi wake walifanikiwa kumtorosha.
Zilisema kuwa kiongozi huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kutumia usafiri wa pikipiki huku akiingizwa kwa kutumia geti la nyuma la hospitali hiyo.
Hata hivyo taarifa hizo zilisema kuwa Sheikh Ponda aliondolewa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kukimbizwa kusikojulikana.
Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa taarifa nyingi zimeenea lakini wao kama Jeshi la Polisi hawana taarifa za kiongozi huyo kupigwa risasi.
Shilogile alisema kuwa polisi walikwenda kumfuata wakati gari lake likiwa linasukumwa kutokana na kutafutwa.
“Wakati wanamfuata pale polisi walilazimika kutumia risasi baridi ndipo wafuasi wake wakafanikiwa kumtorosha kwa pikipiki,” alisema kamanda huyo. Majira ya saa 12:00 jana jioni hadi saa nne usiku misikiti mbalimbali jijini Dar es Salaam kulikuwa na vikundi vya waumini wa dini ya kiisilamu wakijadili tukio hilo huku kukiwa hakuna taarifa rasmi za tukio hilo. Hata hivyo alivyo tafutwa mmoja wa waandaaji wa mkutano huo Bwana Dibagula alithibitishia waisilamu waliokusanyika Msikiti wa Kichangani kuwa tukio hilo ni lakweli na sasa Sheikh huyo wamempeleka sehemu ya maficho ambako anafanyiwa matibabu na Madaktari wa Kiislamu.
"Nikweli amepigwa risasi begani ikatokea upande wa pili, tulimpeleka Hospitali ya Mkoa ila hatukuridhishwa kama kutakuwa na usalama na atatendewa haki tukaamua tumuondoe na sasa anapatiwa matibabu sehemu ya mafichoni na sio Hospitali tena kuna madaktari wa Kiisilamu wanamuhudumia. " alisema Dibagula.
 Wakati mijadala ikiendeelea kwenye misikiti ya Magomeni Msikiti wa Mtambani kinondoni ulituma gari maalum kwenda Mkoani Morogoro huku familiayake nayo ikielekea mkoani humo. Taarifa zaidi tunazifuatilia.

No comments: