Saturday, August 10, 2013

TAKWIMU ZITAONGEA KWA SAUTI ZAIDI KULIKO POROJO!

Tunaamini takwimu nyingi zitaongea kwa sauti yenye kusikika zaidi kuliko maneno tu ambayo tuliyokuwa tunayatumia. Kama ilivyonukuliwa kutoka katika Kamusi-elezo ya Kikristo ya Dunia (World Christian Encyclopedia: A Comparative Study of Churches and Religions in the Modern World) ikielezea tafiti ya makanisa na dini katika dunia hii ya sasa inasema:
“…Ukristo umepata upungufu mkubwa wa wafuasi katika pande la magharibi mwa dunia na katika nchi za kikomonisti kwa miaka 60 iliyopita. Katika Muungano wa Kisovieti (sasa Urusi), Wakristo wamepungua kutoka asilimia 83.6 mwaka 1900 mpaka kufikia asilimia 36.1 leo hii. Ulaya na Marekani ya Kaskazini, usaliti kutoka Ukristo kuingia katika dini nyengine au kutokuwa na dini kabisa zimefikia 1,820,500 kwa mwaka.  Hii ni hasara na upotezaji mkubwa….”[1]
Kulingana na jarida la Kikristo, The Plain Truth,[2] ambalo vyanzo vyake ni World almanac na Book of Facts 1935, Reader’s Digest Almanac na Yearbook1983, linatutanabaisha kuwa katika kipindi cha miaka hamsini (1934-1984):
Watafiti wa mambo!
 Kutokana na takwimu tulizozipata katika jarida hilo, kama tukachukua dini tatu tu jedwali litakuwa kama ifuatavyo:
Makala iliyokuwa katika jarida la The Plane Truth la mwaka 1984 ilisema, “Kinyume na kupungua kwa waumini makanisani huku Magharibi, habari zinaripoti mwenendo na maendeleo ya Waislam yaliyo kinyume kabisa na sisi. Uislam unaweza kuwa ndio dini itakayokua na kuenea zaidi duniani….”[3] Na ni kweli kama ilivyotabiriwa, Uislam sasa ndio dini yenye kukua kwa kasi zaidi duniani. Hata Vatikani wanaukubali ukweli huo kuwa sasa Uislam umeupiku Ukatoliki, “Kwa mara ya kwanza katika historia, hatupo tena juu; Waislam washatupiku,” haya yalisemwa na Monsignor Vittorio Formenti katika mahojiano yake na gazeti la vatikani L’Osservatore Romano. Formenti ambaye ndiye mkusanyaji na mpangaji makala katika kitabu cha Vatikani cha kila mwaka alisema Wakatoliki wamefikia asilimia 17.4 ya watu wote duniani- asilimia isiyoongezeka- wakati Waislam washafika asilimia 19.2 sasa.[4] Sanjari na hilo, The World Christian Database (WCD) na wale watangulizi wao World Christian Encyclopedia (WCE – Kamusi Elezo ya Kikristo Duniani) walifanyia utafiti wa idadi ya watu katika masuala ya kidini na kuachia matokeo ya chunguzi zao kwa mara kadhaa. Kutoka katika majedwali ya matokeo yao, malingano ya Ukristo na Uislam katika ukuaji yalikuwa kama ifuatavyo:
[Rejea za takwimu zilizotolewa fatilia katika: Barrett, David B., George Thomas Kurian, and Todd M. Johnson. 2001. World Christian Encyclopedia: A comparative survey of churches and religions in the modern world. New York: Oxford University Press. p 4. Pia pitia, “The List: The World’s Fastest-Growing Religions.” Foreign Policy 14 May 2007.] Akielezea dini zisizikuwa za Kikristo, msimamo wa mtunzi wa WCE ni: “…tunaweza amini kuwa dini hizo ni za uongo na hazifai na tukajaribu kuzivuta katika imani ya Yesu Kristo….”[5] tukiamini kuwa takwimu hizi za ‘dini pingaji’ hazina upendeleo na haziko kwa ajili ya kuwashinda kuwavuta kuingia katika imani ya Yesu Kristo, wacha sisi tuzitumie katika uchambuzi wetu. The World Christian Encyclopedia inatupa idadi ya wote Waislam kwa Wakristo ya mwaka 1900 na ya mwaka 2000. Idadi ya Wakristo mwaka 1900 ilikuwa na 558 056 332 na mwaka 2000 ikawa 2 019 921 366 na idadi ya Waislam katika miaka hiyo hiyo ilikuwa 200 102 284 na 1 200 653 040.[6]
Kanuni rahisi ya kukokotoa asilimia ya ongezeko katika vipindi hivi ni hii ifuatayo:
Sasa, tukitumia takwimu tulizopewa kutoka WCE, tutapata ongezeko la Wakristo kiasilimia litakuwa:
Na baada ya kukokotoa,  ongezeko la Wakristo litakuwa 262% Tukifanya mahesabu hayo hayo kutumia idadi ya Waislam katika vipindi hivyo.
Tutapata ongezeko la Waislam kuwa ni 500%
Bado, Uislam unaongoza kwa kuwa na asilimia 500% na Ukristo kuwa na 262%. Mwaka 1997, mwanatakwimu kutoka US Center for World Mission alisema kuwa kiujumla idadi ya wafuasi wa Kikristo inaongezeka kwa asilimia 2.3 kila mwaka.[7] Kutokana na Ontario Consultants on Religious Tolerance Uislam unakuwa kwa asilimia 2.9 kila mwaka ambaye ni kasi kubwa kuizidi kasi ya ongezeko la idadi ya watu duniani ambayo ni asilimia 2.3 tu kwa mwaka.[8] Tukichunguza na kufikiri kwa makini, hakuna ugumu utakaibukia katika kukubaliana kuwa kwa mwenendo huu wa Uislam, karibuni kitafika kipindi ambacho Uislam utakuwa ushazivuka dini zote ulimwenguni. Mnamo mwezi Oktoba 2009, gazeti la Kenya The Standard liliibuka na makala ilobeba ujumbe: “Mmoja katika kila wanne ni Muislam katika kipindi hiki ambapo wafuasi washafikia bilioni 1.57 duniani.[9] Takwimu hizi ziliwekwa hadharani na Pew Forum on Religion & Public Life katika ripoti yao ambayo inaheshimika kwa machangunuo ya kinagaubaga kuliko zote inazofanana nazo. Kama mwaka 2000, WCE walisema Waislam walikuwa bilioni 1.2 na baada ya miaka tisa tu Pew Forum waseme Waislam washafika bilioni 1.57. vipi idadi ya Waislam itakuwa baada ya miaka hamsini?! Na tusubiri tuone.

Kuyakataa Mabaya na Kuyachagua Mema

Wengi ya hawa waliorudi*katika Uislamu wanayo taarifu katika Biblia yao isemayo “…kuyakataa mabaya na kuyachagua mema”. [Isaya 7:15], lakini bado wameuchagua Uislam. Kitakachojalisha kama chaguo lao ndio bora na jema ni kina cha utafiti walichochimba na mashiko waliyoyashika ambayo kwa kebehi kubwa yanadharaulika na wengine. Ukifikiria kama walitumia sababu, dalili na uwazi wa akili katika tafiti zao basi bila shaka watakuwa wamechagua chaguo zuri kama alivyosema Thomas Jefferson “Sababu na uchunguzi wa wazi ndio njia pekee za kushinda makosa”. Waliupata ukweli kwa kufatilia na kuudadisi au waliamua kukubali (shingo upande) kurithishwa dini na wazazi kama tu vile alivyokuwa mtoto akifyonza maziwa ya mzazi (mama) basi naye akafyonza kila kitu mpaka dini ya mzazi (mama) pia!!? Ni kweli usiopingika kuwa, ukweli siku zote ndio utakaokuweka huru lakini ukweli huo lazima uwe unaokubalika na wengi, hata kama kwa wakati mwengine uko nje ya mipaka ya dini au jamii. Hi ndio sehemu ngumu zaidi kama asemavyo Galileo, “Ukweli wote huwa ni rahisi kuuelewa pale utapogundulika, tatizo ni hapo katika kuugundua”. Inawezekana hawa waliosilimu waliweza kumpata Mungu baada ya kuufata ushauri wa Biblia, “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” [Yeremia 29:13], katika hii sehemu ya mwisho ya mstari yaani “mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote”, ni kumaanisha kutafuta dini ya kweli kwa utulivu, umakini, juhudi na ari ukiondoa upendeleo . . . kama vile kusoma Qur’an aya baada ya aya, na kusoma vitabu vilivyoandikwa na wanazuoni waheshimiwa Wakiislam….Lakini kwa bahati mbaya hitajio la ukweli ni dogo kuliko usambazaji wake.Lazima utashangaa, sasa vipi mtu anaweza kuwa huru katika kuujua na kuufata ukweli? Wale ambao wanaamua kwa furaha na majigambo kukana kufanya uchunguzi wa ukweli wa Uislam, inabidi angalau wayafikirie maneno ya Joanne Kathleen Rowling, mwandishi wa Kiengereza na mtunzi wa Harry Potter, “Kutofautiana na kutelekezwa kwa dharau huwa inaleta madhara makubwa kuliko hata kutopenda (chuki) kabisa”. Labda hawa waliosilimu walikuwa na aina ya uhuru iliyozungumziwa na C. Wright Mills wakati aliposema, “Uhuru sio kabisa ile nafasi ya kuchagua kile utakacho, wala pia sio ile nafasi ya kuchagua baina ya pande mbili bali uhuru ni kwanza kabisa ni ile nafasi ya kujitengenezea machaguo, kuyajadili na halafu ndio uchague.
Wakati tukisema watu wanazidi kuupokea Uislam siku hadi siku huwa tunamaanisha na kuongelea wasomi wa Ukristo, matajiri, watu maarufu, watu wenye nguvu, wasomi wakubwa, masista wa kanisani, wachungaji, wenye kushawishi watu kuingia Ukristo (evangelicals), marabi, na wale wachaji Mungu katika dini tofauti tofauti bila kuwasahau wale wasio na uwezo katika jamii.* Kuongezea nguvu yaliyosemwa hapo juu, tafiti Fulani ya waliobadili dini kuingia katika Uislam kama ilivyoripotiwa na gazeti la The Sunday Times la 22 Februari 2004 inaonesha wamiliki ardhi wakubwa wa uengereza, watu mashuhuri na watoto wa wakubwa wameupokea Uislam baada ya kuvunjwa moyo na maadili ya kimagharibi.[1] Kiufupi, watu kutoka nyanja zote za maisha, huwa wanaamua kuukubali Uislam bila jitihada kubwa wala shughuli kubwa za kimishenari.
Kiuhalisia, ni Waislam wachache mno wanaoweza kuuacha Uislam kwa ajili ya Ukristo au dini nyengine. Wengi wa hawa waasi wa Uislam, huwa ni ama wazaliwa katika Uislamu lakini wasioijua dini ya Kiislam (wajinga) na hawajajifunza; wafuasi wa madhehebu potofu ya Kiislam; waliotawaliwa na kushawishika na vitu vya kidunia; wasio na mazingira ya kuusoma Uislam; masikini ambao hawana jinsi ila kuvutika kupitia msaada wa msamaria wa Kikristo; wale ambao “…Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na masikio yao na macho yao. Na hao ndio walio ghafilika.” [Q 16:108] na wale wanarubuniwa kiakili. Kwa kulinganisha, wasio Waislam ndio wengi wanaoingia katika Uislam kuliko hao Waislam ambao ni nadra kuwaona wakiaacha dini yao na kuingia nyengine. Cha kushangaza sasa, huwezi kusikia mcha Mungu, mfuasi, sunni wa Kiislam aliyeshiba maarifa ya Uislam akiiacha dini yake eti kwa ajili ya dini nyengine. Ukijumuisha fedha zote walizo nazo, njia na uwezo wa kisasa, na zenye mipangilio mizuri watumiazo katika shughuli na jitihada zao za kimishenari, bado Ukristo hauwezi kuwaopoa Waislam katika dini yao kama vile Waislam wanavyowakomba Wakristo. Sanjari na hilo Peter Kreeft, mtetezi wa Kikatoliki, profesa wa falsafa katika chuo cha Boston na The King’s College, mtunzi wa vitabu zaidi ya 45, msomi na mzungumzaji anayehitajika katika makongamano mbalimbali, na pia ni mjumbe wa bodi ya ushauri wa Kituo cha Watoa Elimu cha Kikatoliki (Catholic Educator’s Resource Center) anasema: “Uislam una kiwango kidogo cha kupoteza waumini wake na kiwango kikubwa sana cha kuingiza waumini”.[2] Hilaire Belloc (1870-1953) ni Mkatoliki, mwanahistoria mzawa wa Ufaransa, na mmoja kati waandishi wenye vitabu vingi Uingereza alikumbana na kimbembe cha ugumu wa kuwatoa Waislam kutoka katika dini yao, hiyo ikiwa ni mnamo mwaka 1938:
Uislam ni dhahiri haubadilikiki. Jitihada za kimeshenari zilizofanywa na Wakatoliki ambazo zimekuwa na dhima ya kuwahamisha wafuasi wa Muhammad kwenda katika Ukristo kwa miaka takriban 400 kwa hakika zimefeli. Tumeweza kumuondoa kiongozi wa Kiislam baadhi ya sehemu na hivyo kuwarudisha watu wetu waliokuwa wametawaliwa na viongozi kama hao wa Kiislam, lakini tumeshindwa kuwavuta wale Waislam* wenyewe mmoja baada ya mwengine….”[3]

 REJEA

* Ingekuwa haturithi dini kutoka kwa wazazi wetu, ipi unafikiri ingekuwa dini yetu ya kufata? Bila shaka tungeifata ile dini inayokubaliana na sheria za kuzaliwa za Mungu kwa binadamu. Sasa kama umerithi kutoka kwa wazazi ubudha na ukaamua kuingia katika Uislamu basi utakuwa umerudi katika dini yako ya asili. Kutoka katika vyanzo vya Kiislamu, kila binaadamu huwa anazaliwa Muislam, na ndio maana tumetumia neno kurudi katika Uislamu. Mtume alisema, “Hakuna mtoto aliyezaliwa ila alikuwa Muislamu kisha ni wazazi wake ndio wanaomfanya awe myahudi, mnaswara au mshirikina.”[Muslim, Bk. 33, No. 6426]. Ali Mazrui, mwanasayansi mashuhuri wa siasa anaandika,”…Marekani kwa mara ya kwanza wamechagua mtoto wa Muislamu kuwa Rais. Hivyo ndivyo alivyokuwa baba yake japokuwa alikuwa mlevi. Hii inamaanisha Obama alizaliwa kama Muislamu japo baadae akalelewa Kikristo…” Tazama Mazrui, Ali. “Obama has chance to mend US-Muslim relations.” City Press 13 Dec. 2008.
*  Ikumbukwe kuwa wengi kati ya wafuasi Muhammad walikuwa ni wale watu wa chini katika jamii mathalan watumwa, mafukara, wanaokanyagwa na wengineo. Na mfano huu umezungumziwa na Heraclius katika kuujua ukweli wa dini. Hivi ndivyo Heraclius alivyodadisi: “Nilipokuuliza ‘Je wengi wanaomfuata huyo Mtume Muhammad ni maskini au matajiri?’ Ukajibu kuwa ni masikini ndio wanaomfuata. Ama kweli, wafuasi wa Mitume wa kweli walikuwa ni masikini.” [Angalia, Bukhari Vol.4, Book 52, Hadith Number 191.]
[1]. Hellen, Nicholas and Christopher Morgan. “Islamic Britain lures top people.” The Sunday Times 22 Feb. 2004. Also see: Whittell, Giles. “Allah Came Knocking At My Heart.” The Times  7 Jan.  2002.
[2]. Kreeft, Peter. “Comparing Christianity & Islam.” National Catholic Register May 1987.
* Uislam ndio dini pekee yenye lisilotokana na mtu au kabila. Uislam una maana ya kunyenyekea kwa Allah tofuati na ukrtsto ulioitwa baada ya Yesu kristo, Budha baada ya Gotama Buddha, Ukonfyushasi baada ya kumfata mwanafalsafa wa kichina Confucius, Umaksi baada ya kuwa wafuasi wa Karl Marx. Na hata dini kama Uyahudi na hindu ni baada ya ya makabila ya uyahudi na uhindi.

No comments: