Thursday, November 20, 2014

BALOZI SEIF AENDELEA NA ZIARA YAKE NCHINI CHINA.

Makamu wa Rais wa Kiwanda cha Dawa za Binaadamu cha Shuangcheng Bwana Jianlin Yuan akimweleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na  Ujumbe wake wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiwa katika ziara ya Kiserikali Katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan.
Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika  kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Zanzibar na Uongozi wa Manispaa ya Mji wa  Haikou ukiongozwa na Meya wa Mji  huo Mstahiki NI Qiang.
Ujumbe wa Zanzibar Ukiongozwa na Makamu  wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif ukifanya mazungumzo  na Ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji vitega uchumi katika  Jimbo la Hainan ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara  ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya Hainan.
Mwenyekiti wa Kiwanda cha kusindika bidhaa za nazi pamoja na matunda  kilichopo Haikuu Huang Chunguang akimfahamisha Balozi Seif na Ujumbe juhudi zinazochukuliwa na Kiwanda hicho katika kulitumia vyema zao la nazi.

No comments: