Wednesday, November 19, 2014

MAPAMBANO YA UKIMWI KWA WATOTO!. Hadi sasa watoto wenye maambukizi ya VVU 130000 wameweza kufikiwa kati ya hao 39317 wamepewa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Baadhi ya wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi wakimsikiliza Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati akifungua  kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF)
Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mbando wakati wa kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto linalofanyika  katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF).
Baadhi ya wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi wakimsikiliza Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati akifungua  kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF).
Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments: