Thursday, November 20, 2014

MIZENGO PINDA NA WENZAKE WASITUDANGANYE...!

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.
Na Julius Mtatiro
Hatutakubali kula peremende. Tunataka bunge lisimamie uwajibikaji mkubwa. Haiwezekani mchezo huu wa kuiba fedha za wananchi unaendelea Tanzania halafu wezi wa fedha hizo wanaishia kujiuzulu tu..Hatukubali.
Lazima bunge lichukue uamuzi mgumu. Lazima waziri mkuu apumzike, Baraza la mawaziri livunjwe, serikali iundwe upya na isimamie jukumu la kuwapeleka mahakamani raia na viongozi wote waliohusika ama kufanikisha au kupokea mgao wa fedha za ESCROW.
Na kisha pamoja na kuwashtaki, lazima hasa warejeshe fedha hizo, kisha wakapumzike kwenye magereza zetu bora.PERIOD!
Supu ya mbwa hunywewa ikiwa ya moto IPTL and Escrow. BRING BACK Our MONEY.

NIMEITOA KWENYE FB WALL YA Josh Nassari: IPTL SAGA UPDATES:
Katika kikao chao kilichoisha muda wa saa tisa na dakika kama tano hivi leo alasiri, baraza la mawaziri lililokutana ghafla chini ya waziri mkuu Mizengo Pinda limekumbwa na mtafaruku mkubwa kutokana na kashfa ya IPTL inayofukuta kwa kasi.
Katika kikao hicho mawaziri wamewalazimisha mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredrik Werema na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini bwana Eliakim Maswi kuachia ngazi kwa uzembe huku Prof. Tibaijuka akitakiwa kuwajibika kwa kukiri hadharani kuwa alipokea shilingi bilioni moja za kitanzania kutoka kwa mbia wa IPTL.
Hii imelazimishwa ili kulinusuru baraza zima la mawaziri pamoja na Pinda ili kuufanikisha mpango wa ripoti hiyo kuzuiwa isifike bungeni kujadiliwa.
Aidha hali hiyo imesababisha hisia kali miongoni mwa mawaziri ambapo naibu waziri Godfrey Zambi pamoja na Werema walitoleana maneno makali nusura kukunjana!
Pia imedaiwa kuwa tayari Prof. Tibaijuka amekubali kuwajibika huku wengine wakitia ngumu!

No comments: