Thursday, November 13, 2014

TIGO WELCOME PACK KUHAMIA KANDA YA ZIWA!

WASANII wachekeshaji wa kundi maarufu nchini la Orijino Komedi, wanatarajia kufanya tamasha kubwa Kanda ya ziwa lililoandaliwa na Kampuni ya Tigo lijulikanalo kwa jina la Welcome Pack. Tamasha hilo linalowapa wananchi fursa ya kina kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo litafanyika jijini Mwanza Jumamosi hii. Mbali na kundi hilo wasanii wa Hiphop Farid Kubanda Fid Q, Young Killer na Hamisi Mwinjuma Mwana FA, watatumbuiza pia kwenye tamasha hilo. Kutoka kushoto, Wakuvwanga, Joti na Masanja.
Meneja wa Bidhaa wa Kampuni ya Tigo Edwin Ngoa (kulia) akiwa na wasanii Masanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi (wapili kulia) Wakuvwanga, na Young Killerwakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha maalum lililoandaliwa na kampuni hiyo na kupewa jina la Welcome Pack, ambapo mbali na kundi hilo kwenye tamasha kutakuwepo na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Faridu Kubanda Mwana FA na Young Killer. 
Fid Q, (kulia) akiburudisha kwa kuimba.
Songi la Fid Q lawatuliza Orijino Komedi.
Mwanaumeeee!
Joti nae akafanya vituvyake mbele ya waandishi wa habari.
Masanja hakukubali kuzidiwa na Joti nae akashusha Mzigo mpya!
Akamilizia! Yaaaakheeeeeeeeeeeeeeeeeee!
Young Killer, akitibu mbavu kwa vichekesho vya joti!
Mwana FA, Hakuwa nyuma nae akatema mistari.
Joti akimsaidia Mistari Young Killer.
Timu Mzima itakayokonga Nyoyo za wakazi wa Kanda ya ziwa.

No comments: