Monday, November 10, 2014

VIONGOZI WA MIKOA NA WILAYA ZANZIBAR WANOLEWA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir wakati alipowasili katika Hoteli ya Sea Cliff kufungua semina ya siku tatu ya Viongozi wa Juu Mikoa na Wilaya za Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Abdulrahman  Ghasia, alipowasili katika viwanja vya Sea Cliff Mangapwani Mkoa wa Kaskazini B Unguja leo alipofika kufungua semina ya Viongozi wa Juu Mikoa na Wilaya za Zanzibar
Baadhi ya wakuu wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika ufunguzi wa semina na ya siku tatu iliyowashirikisha makatibu tawala wa Mikoa ya Zanzibar na baadhi ya Tanzania Bara iliyoanza leo katika ukumbi wa Sea Cliff nje kidogo ya Mji Zanzibar.
Washiriki wa katika semina ya Viongozi wa juu wa Mikoa na Wilaya za zanzibar na Baadhi kutoka Bara wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipotoa hutuba yake ya ufunguzi wa semina hiyo leo katika Hoteli ya Sea Cliff  Kama nje ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa semina ya Viongozi wa juu wa Mikoa na Wilaya za zanzibar na Baadhi kutoka Bara inayohusu Mahusiano na mwingiliano katika siasa na utendaji kwa Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa mikoa ya zanzibar na baadhi Tanzania Bara leo katika Hoteli ya Sea Cliff  Kama nje ya Mji wa Zanzibar.Picha zote na Ikulu

No comments: