Wednesday, November 26, 2014

WIZARA YA MAMBO YA NDANI WAJINOA ARUSHA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil    wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw.Adoh Mapunda muda mfupi kabla ya Bw. Mapunda kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichoanza leo jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Mbarak Abdulwakil (watatu kutoka kulia) akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha  Bw. Adoh  Mapunda (kushoto) kwenda kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichoanza leo jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs, wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Kaniki anayefuatia ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Sylivester Ambokile . 
Wakiimba wimbo wa Solidarity  Forever pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Solidarity  Forever
Peter Mbelwa  kutoka Mamlaka ya Kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akitoa mada kuhusu Maandalizi ya kustaafu katika kikao cha  Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kinachoendelea jijini Arusha katika hoteli ya Corridor Springs.                                         

No comments: