Wednesday, November 19, 2014

ZIARA YA KINANA LINDI

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) baada ya kupokewa na mamia ya wananchi jimboni humo kufanya ziara ya kuimarisha chama wilayani humo. Kinana na msafara wake alitembelea miradi ya mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana akilima shamba kwa kutumia treka katika shamba la ufuta lililopo katika Kijiji cha Mkotokuyana, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, pembeni yake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe maybe alikuwa anashuhudia tukio hilo la ulimaji. Kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Kinana alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya wananchi wa jimbo hilo baada ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana (hayupo pichani) kumpa nafasi ya kuzungumza na wananchi wake. Chikawe alisema tangu alipoanza kuliongoza jimbo hilo mwaka 2005, shule za sekondari zilikuwa tatu na mpaka sasa zipo 26. Pia jimbo lake sasa halina shida ya maji baada ya kuzinduliwa mradi mkubwa wa maji jimboni humo. Kinana pamoja na msafara wake wapo mkoani Lindi katika ziara ya kuimarisha chama pamoja na kutembelea miradi mbalimbali maendeleo. 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa mjini Nachingwea kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika Jimbo hilo pamoja na changamoto mbalimbali zinazozikabili jimbo hilo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe ambaye aliitwa kwa ajili ya kuwafafanulia masuala mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya tangu alipoanza kuliongoza jimbo hilo. Mamia ya wananchi waliudhuria mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika mjini Nachingwea. Picha na Felix Mwagara

No comments: