Friday, December 12, 2014

BALOZI WA MAREKANI AMTEMBELEA CHIKAWE!

Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na wizara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) pamoja na maofisa wa ubalozi huo, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe na Balozi huyo walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini.

No comments: