Thursday, December 18, 2014

DK.SHEIN AZINDUA UMEME DONGONGWE UNGUJA.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akihutubia wananchi wa Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini  Unguja katika sherehe za Uzinduzi wa Umeme Kijijini hapo leo. Kushoto Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mohamed Seif Khatib (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdalla Ali. 
Akihutubia mbele ya wananchi.
Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, kuzungumza na wananchi baada ya kuzindua rasmi nishati ya Umeme katika Kijiji cha Dongongwe Wilaya ya Kati Jimbo la Uzini Mkoa wa Kusini Unguja leo.Picha na Ikulu.

No comments: