Friday, December 12, 2014

MIAKA 16 YA LUIZA MBUTU KWENYE MUZIKI!

Luiza Mbutu kazini.
KIONGOZI wa bendi  mpya  pia mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Hamza Kalala ‘Komandoo Hamza kalala ama unaweza kumwita mzee wa madongo’ amethibitisha kushiriki katika onyesho maalum  la miaka 16  ya mwanamuziki Luzer Mbutu.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya  The African  Stars Entertainment (ASET)  Asha Baraka alisema Komandoo tayari amethibitisha hivyo usiku huo utakaofanyika  Desemba 20 ndani ya ukumbi wa Mango Garden utakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakongwe.
Pia alimtaja Stara Thomas ‘Stara T’ , Siza Mazongeza’ Mamaa wa Segere’, pia wanafanya mazungumzo na wasanii mbalimbali ambao waliwahi kufanya kazi na Mbutu tangu bendi  hiyo ilipoanzishwa  kama vile Bob Gaddy, Banza Stone, Adolph Mbinga  na wengineo.
Akizungumza jana na Tanzania Daima Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Asha Baraka alisema kuwa wameandaa onyesho hilo ambalo litakua maalum kwa Kiongozi wa bendi hiyo ambaye anaetimiza miaka 16 ndani ya bendi bila kuhama tangu ilipoanzishwa.
“Uongozi wa ASET umeamua kuandaa usiku maalum wa kumuenzi Luiza kutokana na kua na msimamamo wa kukaa katika bendi kwa muda wote huo bila kuhama hilo ni jambo la kujivunia” alisema Asha.
Aliongeza kwa kusema kuwa onyesho hilo litakwenda kwa jina la Luiza Mbutu na Twanga Pepeta ambalo pia kutakuwa na shamrashamra zake ambazo zitatajwa siku itakapowadia” alisema Asha.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa wao kama ASET wanatambua mchango wa Luiza ndani ya bendi hiyo hivyo kutakuwa na tukio laaina yake ambalo mashabiki na wadau wa bendi hiyo pamoja na wapenzi wa Luiza wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia litakalojiri sambamba na kupata burudani kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta.

.Kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

No comments: