Sunday, December 7, 2014

WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKIANA NA WAGOMBEA SERIKALI ZA MITAA KUPIGA KAMPENI YA NYUMBA KWA NYUMBA JIMBONI NACHINGWEA.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Libundu, Kitongoji cha Nangote, Kata ya Kiparamnero wilayani Nachingwea katika Kampeni ya nyumba kwa nyumba ya kuwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa Serikali za Mitaa wilayani humo. Waziri Chikawe aliwaomba wananchi wa Nachingwea kuwapigia kura viongozi hao waliopitishwa na CCM kugombea nafasi hizo walizoomba. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu nchini. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akimtambulisha kwa wananchi (hawapo pichani), Dastan Likwama ambaye anagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nangote katika Kata ya Kiparamnero waliohudhuria Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika kitongoji hicho. Waziri Chikawe aliwaomba wananchi hao kumpigia kura kiongozi huyo aliyepitishwa na CCM kugombea nafasi hiyo. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu nchini. Picha zote na Felix Mwagara. 

No comments: