Sunday, December 7, 2014

SHAMRA SHAMRA ZA UHURU WA TANGANYIKA.

Waziri wa Fedha na Uchumi Saada Mkuya Salum, akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru Afisa Mawasiliano Msaidizi wa Benki ya Posta Tanzania Chichi Banda, wakati wa tamasha la kutangaza mafanikio ya serikali ya awamu ya nne sambamba na maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum, akiwasalimia wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Sigara Chang'ombe jijini Dar es Salaam, hadi siku ya kilele cha sherehe za Uhuru wa Tanganyika Tar 9 Disemba mwaka huu.

Wafanyakazi wa Serikali ambao wengi wao ni wa wizara ya fedha na Uchumi wakiburudika na bendi ya Msondo Ngoma.
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa kwenye banda lao.
Wasanii wa kikundi Cha Ngoma za asili Cha Hisia Vijana wa Kazi nao walitumbuiza kwenye Sherehe hizo.
Kiongozi wa nyimbo za kikundi hicho.

No comments: