Sunday, December 7, 2014

Wenger:Safu ya ulinzi ilikuwa maji maji.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger.asema kuwa safu ya ulinzi ya Arsenal ilikuwa lege lege walipochapwa mabao 3-2 
Safu ya ulinzi ya Arsenal ilikuwa ''maji maji'' sana dhidi ya Stoke wakati timu hiyo ilipolazwa kwa mabao 3-2 katika uwanja wa Bitania ,kocha Arsena wenger amesema.
The Gunners ilifungwa mabao matatu katika kipindi cha kwanza ,ikiwemo bao kwanza baada ya sekunde 19 kabla ya kuanza kuvamia lango la Stoke ili kulipiza.
Nadhani tulikuwa hatuna uzoefu wa siku nyingi katika safu ya nyuma,alisema.
Hatukuweza kuwachezesha Laurent Koscielny ama Nacho Monreal na nadhani tulikuwa ''lege lege'',kuhimili walichotukabili nacho.
Koscielny aliyeanza mechi mbili zilizopita alipumzishwa huku Monreal akiwa na jeraha.
Kierran Gibs alicheza kama beki wa kushoto naye calum Chamber akisaidiana na Per Mertesacker katika safu ya Ulinzi huku mchezaji mwenye umri wa miaka 19 hector Bellerin akianzishwa kama beki wa kulia.

No comments: