Wednesday, January 28, 2015

Unyama waliofanyiwa CUF huu hapa! Polisi walikusudia kuu!

Jamaa huyu alikula mkong'oto huku mkonowake ukiwa umefungwa na pingu kwenye Difenda,kundi hili la Polisi hawa wenye silaha wakipambana na mtu mmoja ambae hana silaha.
Wakiendelea kumkung'uta!
Mwenyekiti wa CUF mwenye (Tshirt nyekundu) akizingukwa na walinzi wake huku polisi wakimtaka kumkamata lakini hawakufanikiwa hadi alipoamua mwenyewe kwenda kwenye gari la polisi. Mwenye Tshirt  ya njano ni moja na mwenzake ni moja ya askari walikuwa wakitaka kumkamata Lipumba.

Huyu nae alipigwa mweleka na kutumbukia kwenye mtaro.
Akiondolewa kwenye Mtaro.
Mmoja ya wanachama wa CUF Mbarara Maharagande akiwasihi polisi waache kuzuia maandamano yao kwani watasababisha vurugu isiyo na lazima.
Bango la Tahadhari.
Mvutano kati ya Askari na walinzi wa Prof. Lipumba.
Blue Guard wa CUF walipofanikiwa kumuokoa Lipumba mikononi mwa polisi kabla hajaamua mwenyewe kujipeleka.
Baada ya kufanikiwa kumnasua mipango ikaendelea "tuendelee ama tusiendelee!
Mwandishi wa habari na Mpiga Picha wa Gazeti la Jambo leo Hamisi akishikiliwa na Polisi pamoja na Kamera yake akiendelea kupiga picha akiwa ndani ya Defenda ya Polisi.

Dereva wa Gari la CUF akila kipigo.
Askari karibu wanane wakimvamia Dereva wa gari hilo la CUF na kumpiga.
Kundi hili nalo likimtesa mwanachama mwingine wa CUF ambaye alikuwa tayari amejisalimisha kwa polisi.
Wakati Prof.Lipumba akishuka kwenye gari lake ili aende kwenye Difenda  Polisi wakaanza kumvamia mlinziwake na kupiga virungu huku lipumba akishuhudia.
Lipumba akiwa Mahakamani kusomewa mashitaka ya kesi ya Uchochezi na Vurugu.
Akiteta jambo na Mawakiliwake Kisutu leo jijini Dar .
Wafuasi wakifurahi baada ya Lipumba kupata dhamana Mahakamani Kisutu jijini Dar leo.


Waliokamatwa waliachiwa Wote, Baada ya kusikia Suala limefika mjengoni wkamgeuzia kibao Lipumba na kumfungulia kesi ya uchochezi wa vurugu.Lipumba Acheki afya St. Peters, asema yuko Ngangari.

No comments: